UJUMBE UNATOKA: ISAYA 48:17-18
Bwana, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye ili upate FAIDA, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata. Laiti ungalisikiliza AMRI zangu! Ndipo amani yako ingalikuwa kama mto wa maji, na haki yako kama mawimbi ya bahari.
tAFAKARI:
Siku za hivi karibuni nilimsikia kijana mmoja wa kiume akimwambia mwenzie akisema “Tafakari anayotoa huyu mzee mimi sitaki kuisoma, utafikiri ananisema mimi tu” moyoni nikacheka nikajifanya sijasikia, na ni wengi wakifungua email zao wakiona tu NENO LA LEO wana “delete” hawataki hata kusoma, na wengine wanasoma ila hawazingatii. Rafiki yangu kijana, Neno la Mungu ni Upanga unaogawanya Nafsi (Mwili) na Roho, ukiona unasoma neno linakukosoa, na linakuuma moyoni, mshukuru Mungu, hiyo ni sauti Mungu inakuonya, fanya uamuzi wa kutii neno lake. Ibilisi ndiye anayewaongoza watu kuchukia ukweli wa neno la Mungu ili baadaye awatese na hatimaye kuwaua kifo kibaya. Wewe mwenyewe ni shahidi ni faida gani umeipata kwa dhambi uliyoitenda? Ni kujilisha UPEPO usio na faida.
Katika tafiti zilizofanyika; Changamoto kubwa zinazowakibili vijana ni maswala ya Mahusiano yaani; Marafiki (Mapenzi), Uchumba na Ndoa. Swala hili la Mahusiano katika kizazi chetu cha sasa limekuwa na sula tofauti, zamani mtu akiingia kwenye mahusiano ilikuwa ni Baraka ya kudumu katika maisha, lakini siku hizi mambo yamegeuka, kijana akijiingiza kwenye mahusiano ni sawa na kubeba Bomu la Nuclear ambalo kila wakati anakaa kwa tahadhari hajui litapasuka lini. Vilio, Kuvunjika moyo, kukata tama, kuchanganyikiwa, kujiua, kujijutia, manung’uniko, makelele, magonvi, dhuluma, kuoneana, kuachana Solemba n.k. ndiyo sehemu ya maisha. Hata wanaofunga ndoa siku hizi, furaha zao ni za kitambo tu, baada ya hapo ni Majuto, kwa sababu mwanzilishi wa mahusiano yao ni Ibilisi aliyewaongoza kukidhi tama za miili yao, sio upendo wa Mungu.
Jambo la pili ni Ugumu wa Maisha, yaani kupata pesa za kutosha kupata mahitaji mfano. Kununua gari, kustarehe, kulipa pango, kujenga, kula, kuvaa, kulipa ada ya chuo n.k. Siku hizi kuna Majimama (Sugar Mumy) wenye pesa, vijana hawaoni wala kusikia, hata kama wanaogelea mabwawa marefu ya majimama, hawaangalii ili mradi mkono uingie kinywani, ikitokea wameoa vijana wenzao inakuwa ni usumbufu tu usiokoma. Hatuwasahau Majibaba wanaoitwa Mapedeshee, Mabuzi au ma ATM n.k. Vijana wa kike kutokana na maisha kuwa magumu wameamua kubeba hata mizigo isiyostahili yao. Binti mmoja alifiwa na Mwanaume kifuani akiwa anavunja Amri ya Uzinzi guest house, Kumbe buzi lenyewe gari lake ni afadhali gari la Mkaa, haliwaki mpaka uskume (kwa booster za kimasai). Binti akiolewa na kijana naye inakuwa ni taabu, make alizoea kuendesha Magari ya Mizigo, halafu anajikuta anaendesha Bajaji au gari aina ya Epsi.
Vijana sio waaminifu kabisa, anakuwa na Wachumba, anakuwa na ATMs, na anakuwa na watu wa kula nao BATA. Hivi unategemea ndoa itakuwa na sura gani? Vijana! Katika tafakari ya leo, Mungu anasema “Mimi ni Bwana Mungu wako nikufundishaye ili upate FAIDA, Laiti ungelisikiliza AMRI zake, ndipo AMANI yako ingalikuwa kama mto wa MAJI na HAKI yako kama mawimbi ya Bahari”. Kijana unataka AMANI moyoni? Unataka FAIDA au Mafanikio katika mambo yako? Geuka sasa, mtazame Yesu Kristo, yatosha kumtumikia Shetani kwa maisha ya dhambi. Neema ya Yesu ipo kukuokoa na kukupatia Ushindi wa Dhambi.
MUNGU WA AMANI AWAPATIE SIKU NJEMA YENYE BARAKA TELE.
Ev: Eliezer Mwangosi.
0755808077 & 0652571733
No comments:
Post a Comment