Ujumbe wa leo unatoka – Yeremia 29:11,
“Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya AMANI, wala si ya mabaya, kuwapa ninyi TUMAINI, siku zenu za Mwisho”
TAFAKARI:
Vijana na Wazazi ambao ni washauri wa Vijana, inahitaji kutumia akili kidogo sana kuthibisha kuwa Ulimwengu wetu sasa uko taabani, angelikuwa ni binadamu tungesema yuko mahututi karibu kukata Roho. Hata hivyo Mungu anafanya kila njia ili watu waishi kwa AMANI na MATUMAINI katika hali ambayo wengi wamejikatia tama. Kuna usalama kusimama upande wa Mungu, zaidi ya hapo ni kukinywea kikombe – Siku ambayo Sukali itageuka kuwa dawa ya Mwarobaini au TAMU kuwa CHUNGU.
Leo nimeamua kujibu baadhi ya Maswali waliyoniuliza Vijana:
1. Ni umri gani Mzuri wa kuoa au Kuolewa?
- Kwa Mwanaume ni kati ya Miaka 25 hadi 35, na Mwanamke ni Miaka 20 hadi 30. Miaka hii ni wastani wa wanandoa kuwa na Muda mzuri wa Kuzaa, na kulea watoto hadi kuwasomesha, na hatimaye na wao kuanza maisha bila matatizo.
Watoto hawatakuita BABU au BIBI, Mwanamke utakuwa na Muda Mzuri wa Kuzaa, mtakuwa na nafasi nzuri ya kuzaa kwa mpango. N.K.
2. Ni vizuri Mume na Mke wapishane miaka Mingapi?
Kuna usemi vijana wanasema ng’ombe hazeeki maini na wengine wanasema “Age is just Numbers”. Vyovyote watakavyosema, kuna athari nyingi kama utaamua kuingia katika ndoa bila kujali Umri “Age Gape”. Ushauri wa kitaalamu na kisikolojia – wastani wa miaka ya kupishana ni Miaka Mitano hadi Kumi, Ibrahimu alimzidi Sarah Miaka Kumi [ Mwanzo 17:17 ].
- Vijana mnaofugwa na Majimama (Sugar Mamy), mmtegwa kwa shida za maisha, kwani hata hivyo macho hayakomi kutamani maua yanayochipuka – Outing vipi inakubali? Kama ndio, hiyo ni ya kitambi muda si mrefu utamkimbia akiwa kibogoyo.
- Na Mabinti wanaokubali mizigo inayowazidi, yaani kuolewa na Wazee wana hasara kubwa, kuna siku Gari litazimika hata ukilisukuma halitawaka. Hiyo ni sawa na GARI LA MKAA KUWAPANDISHA WATALII, yaani ni kero tupu, wengi wanadanganywa na Vijisenti ambavyo mara nyingi havidumu.
Kuna maswali Mengi na Mashauri Mengi ila Muda hautoshi. Tutaendelea wiki ijayo na ninapanga kuwa na semina ya Ushauri kwa Vijana. Kumbuka Mungu anawawazia Mawazo ya AMANI katika Maisha yenu, ukimtegemea atakupatia Mwenzi wa kufanana naye.
MUNGU AWABARIKI NA KUWAPATIA SIKU NJEMA YENYE MAFANIKIO TELE
Ev. Eliezer Mwangosi
No comments:
Post a Comment