“Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, kwa paa na kwa ayala wa porini, msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe”
TAFAKARI:
Kama
kuna janga la HATARI ambalo jamii ilipaswa kulitangaza kwa siku za leo,
ni Vijana kujihusisha na mapenzi kwa wakati usioruhusu. Katika tafakari
za nyuma niliwahi kutoa somo la “Kila jambo lina wakati wake”. Swala la
Mapenzi katika kizazi chetu limekuwa tishio, Kuna dada mmoja ambaye
alikatisha masomo ya chuo kikuu kwa kuvurugikiwa na akili, kwa sababu ya
mawazo mengi baada ya kuachwa na BOYFRIEND wake, hadi leo yuko nyumbani
kama zezeta.
Mapenzi
ni Moto ambao ukichochewa sio rahisi kuuzima mpaka utimize kusudi lake
la kuteketeza, Mapenzi yanalewesha na kupiga upofu, ukinaswa na Upendo –
Mtu Kipofu utaona ana makengengeza, Mwenye mapengo unaona ana Mwanya,
yaani ukipenda hutaona Kasoro. Neno linasema “UPENDO una nguvu kama Mauti … Ni kama MOTO ambao hakuna maji yanayoweza KUUZIMA” Wimbo ulio bora 8:6-7.
Ndio maana utakuta kijana anaogelea kwa Bibi kikongwe, hebu jaribu
kumwambia huyo hakufai, atakuwa tayari kujiua, make yeye anamuona ni
Binti wa Umri under eighteen.
Ushauri
wangu kwa Vijana ni Huu – Mungu ameweka Upendo ndani ya Mtu kwa
makusudi ya KUDUMU, sio wa kuishia njiani au kuvunjika. Hivyo kabla
hujaingia katika mahusiano ya Mapenzi na Mtu yeyote Mwambie Mungu
akupatie the “Right Person at the Right Time”.
Jamii yetu inaendelea kuathirika kwa ongezeko la Vijana wenye Misongo,
inayotokana na vurugu za Mapenzi yasiyo na mpangilio. Shetani
amefanikiwa kuteka vijana wengi – akiwatilia Sumu kwenye Sukali ya
Mapenzi hata hawasikii ushauri.
Biblia
inasema Ngono nje ya Ndoa ni UZINZI NA UASHERATI. Vijana asilimia kubwa
wameziba masikio wasisikie neno la Mungu, naye Mungu anaziba masikio
asisikie vilio vyao [Isaya 59:1-2] wanapokuwa
wametelekezwa na matapeli wa Mapenzi. Bado Mungu anawataka vijana
wafanye uamuzi upya wa kusimama Upande wake ili awapatie RAHA nafsini
mwao sasa na hata Milele.
VIJANA NAWAKIA SIKU NJEMA – MUNGU AWABARIKI NA KUWAPA AMANI
Ev. Eliezer Mwangosi
No comments:
Post a Comment