NENO LA LEO: Ayubu 14:1-2
“Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke, siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile UA, kisha hukatwa; hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe”
TAFAKARI:
Rafiki!
Leo tunatafakari juu ya UA, wote tunajua kuwa UA LIKICHANUA
KINACHOFUATA NI KUNYAUKA, na Jambo la kuvutia zaidi ni kuona
linavyopendeza na kuvutia, mbali na wanadamu kupenda MAUA, hata wadudu
pia utakuta wamejazana.
Maisha
ya Mwanadamu ndivyo yalivyo, kama UA linavyonyauka ghafla ndivyo maisha
yanavyokatika, kumbuka sisi sote ni marehemu watarajiwa wasiojua muda
wa kifo.
Vijana!
Mwisho wa UA kuchanua ni kunyauka, wengi huutumia wakati huo vibaya,
HAWATULII, Utakuta Binti mzuri eti anajirusha na Libaba ambalo halina
Mpango wa kumuoa ili mradi ana Vijisenti – Hao ni WADUDU WAHARIBIFU.
Tunaona baadhi ya MAUA yanavyoharibiwa na wadudu waharibifu,
yanatobolewa na kuchafuliwa, ndivyo vijana WANAVYOPOTEZEWA DIRA YA
MAISHA. Akili zikiwarudia na kutaka Kuolewa au kuoa wanajikuta
wamechelewa – UMRI WA KUCHANUA UMEPITA, hata wakitumia MAKE UP,
hazisaidii, wadudu wote wamekimbilia maua mengine yanayochanua.
Vijana!
Habari za ku “PASS TIME” na vija wenzenu kwa maisha ya Ngono, Ulevi,
Muziki n.k. yanawapotezea DIRA ya Maisha, tumeshuhudia wengi wanasukumwa
na TAMAA, na Wengi wanatumika kama VYOMBO vya kukidhi
tama za wengine, mwisho wake ni kuachwa kwenye Mataa. MAISHA YOYOTE YA
DHAMBI NI TANZI YA UHARIBIFU.
VIJANA WENGI WANAJUTIA KWA YALIYOPITA NA WENGINE NDIO WAMEZAMA.
SULUHISHO NI KUMTEGEMEA MUNGU – KWAKE YOTE YANAWEZEKANA
NAWATAKIA SIKU NJEMA NA WEEK END NJEMA YENYE BARAKA TELE
Ev. Eliezer Mwangosi
Mungu akubarikie sana
ReplyDeleteUsichoke kutuelimisha mungu akubaliki
ReplyDeleteKwakutumia kipaji chako chakutuelimisha kwanjia ya maandish
Umefanya vyema kwasababu kwa njia hii kamwe ujumbe hauwez kupotea au kupitwa nawakati
GOD Bless You��
Mungu akubaliki
ReplyDeleteAmen
ReplyDelete