Ujumbe Unatoka: Ayubu 20:12-13, 27
Ingawa
UOVU una tamu kinywani mwake, Ingawa auficha chini ya ulimi wake, Ingawa
auhurumia, asikubali kuuacha uende zake, Lakini akaushika vivyo kinywani
mwake….. Mbingu zitafunua wazi uovu wake, Nayo inchi itainuka kinyume
chake.
TAFAKARI:
Ni
hali ya kawaida katika ulimwengu wa maendeleo kuona vidonge hasa vya kutibu
malaria kuona vimepakwa radha ya sukari kwa nje, lakini kwa ndani ni chungu
ajabu. Siku moja niliona mtoto akilia baada ya kutafuna kidonge aina ya
Comaquine ambacho alipolamba akaona ni kitamu akafikiri Pipi, baada ya kutafuna
ndipo akakutana na Uchungu. Ndivyo ilivyo
kwa mitego ya panya, wengi wanaweka SUMU ndani ya Mchuzi wa Samaki au nyama,
panya anapokula anasikia Utamu mpaka kwenye Kisogo, lakini baada ya muda mfupi
utakuta amekufa bila matumaini.
Wewe
kijana na rafiki yangu unayesoma tafakari ya leo, nataka nikuambie kuwa dhambi
ni tamu lakini ndani yake Adui ameweka Sumu ambayo ni lazima itemize kusudi
lake. Piga picha siku ulipokutana na huyo boy friend au girl friend wako,
ukalegeza macho na kutamka neno “Honey / Sweet I LOVE YOU” ulijisikiaje? Na hatimaye utakuta taratibu
lakini kwa uhakika wanakokotana hadi wanaingia katika Dhambi ya Zinaa. Wengi
hawapendi kuvunja Amri ya Mungu inayosema “USIZINI”, lakini kwa hila za shetani
anawaangusha. Tendo la Ndoa nje ya Ndoa halali ni Dhambi ya Zinaa, hiyo ni
sukari iliyotiwa sumu ya kufisha, inaua taratibu lakini kwa uhakika.
Kijana
mmoja aliyenusulika kufa akiwa amekunywa sumu ya panya akitaka kujiua baada ya
kugundua ameambukizwa Virusi vya ukimwi, tulipomuuliza ilikuwaje? Akasema
rafiki yangu wa kiume alinilazimisha kufanya naye ngono, siku moja alimtembelea
boy friend wake, chumba chenyewe ni kimoja na viti ni kitanda, alipoingia, kwa
maneno ya kubembeleza wakajikuta wamefika kwenye “Point of No Return” wakavunja
AMRI sa saba, ndivyo vijana wengi walivyoanguka bila kutarajia na wanabaki
wakisema “NINGEJUA” lakini wanakuwa wamechelewa.
Neno
linasema, Dhambi ni TAMU na wengi wanajitahidi KUIFICHA ili wasigundulike,
wasije wakaicha, Lakini Mungu anasema; Mbingu zitaifunua na itawekwa wazi. Popote unapokuwa, iwe Guest
House, Chumbani, kwenye vichochoro, hata iwe usiku wa GIZA nene, chochote
unachofanya, Kamera ya Mbinguni inakumulika na kuchukuwa Picha, chicho la BWANA
liko kila mahali likichunguza kila tendo – na mwisho anasema ATAUFUNUA UOVU
HUO.
MUNGU ANATUFUTA VIJANA KAMA AKINA DANIEL KATIKA KIZAZI
CHA LEO WATAKAOSIMAMA KWA UAMINIFU – KWA NINI USIWE WEWE?
SIKU YA LEO IKAWE YA BARAKA NA USHINDI TELE
Ev: Eliezer Mwangosi.
Masomo zaidi: http://emwangosi.blogspot.com/
(VIJANA) http://kayanafamilia.blogspot.com/
(NDOA) http://matengenezo.blogspot.com/
(UKWELI ULIOFICHIKA NA KUUKULIA WOKOVU)